DC MJEMA: WANAWAKE ZIFIKIENI NDOTO ZENU, INAWEZEKANA
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akizungumza na wanawake wajasiriamali katika uzinduzi wa Miradi ya Changamka Mwanamke (Picha na Daud Lyon) Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akizungumza na wanawake wajasiriamali, kuwapa hamasa kuzifikia ndoto zao. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akizungumza na wanawake wajasiriamali, kuwapa hamasa kuzifikia ndoto zao. Na Heri Shaban MKUU wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amezindua miradi miwili ya Taasisi ya Wanawake wa Changamka Mwanamke Dar es Salaam jana ili iwawezeshe Wanawake kujikwamua kiuchumi. Uzinduzi wa miradi hiyo ilifanyika Dar es salaam jana, katika ukumbi wa NSSF ambao ulishirikisha Wanawake wa Changamka Mwanamke Wanawake wa JUKWAA Wilaya ya ILALA na Wajasiliamali. Katika mafunzo hayo alizindua miradi ya kilimo cha pilipili na viti vya kukodi katika shughuli mbalimbali. Akizungumza katika hafla ya taasisi ya Changamka Mwanamke Sophia Mjema alipongeza Changamka Mwanamke kwa kuwaungan...