TANZANIA YA KESHO IPO MIKONONI MWA WATOTO WAKE. TUNAWAANDAJE?

Na Jabiri O. Makame Tarehe 16 Juni, Tanzania inaungana na mataifa mengine Barani Afrika KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA. Siku hii huadhimishwa kila mwaka ikiwa ni kumbukumbu ya vifo vya watoto waliouawa huko sowetho, Afrika Kusini wakiwa katika maandamano ya kupinga utawala wa kibaguzi wa makaburu. Siku hii hutumika kwa kufanya tafakuri juu ya haki mbalimbali za mtoto katika masuala ya malezi, makuzi, ulinzi na usalama wa mtoto. Maamuzi ya kuadhimisha siku hii yalifanyika Novemba, 20, 1989 ambapo mkataba wa Kimataifa wa haki za watoto (Convention on the Rights of the Child) uliridhiwa katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa na Tanzania iliridhia mkataba huu mwaka 1991. Maamuzi hayo yalifanyika kwa kutambua kwamba, hatma ya taifa lolote lile duniani inategemea aina ya malezi na makuzi yatolewayo kwa watoto. Taifa linalojali na linalotambua thamani ya mtoto wa leo kwa mustakabali wa taifa la kesho, daima huandaa mazingira wezeshi ya malezi na makuzi ya mtoto ili ...