NGAZI YA UONGOZI KWA KIZAZI CHA VIONGOZI WA KESHO: Hatua 10 za Kukuza Uwezo Wako wa Uongozi (LADDER OF LEADERSHIP FOR THE NEXT GENERATION LEADERS: 10 Steps to enrich your leaderahip potential)


Kwa miaka kadhaa sasa nimekuwa nikikutana na vijana wenzangu katika matukio mbalimbali kuzungumza kuhusu masuala ya Vijana na Uongozi. Mwaka 2018  nilialikwa na Taasisi ya AmaniFursa katika kongamano liitwalo “Career Building Festival” kwenda kuzungumza na vijana wa sekondari kuhusu “Vijana na Uongozi” Baada ya kutafakari kwa muda kuhusu nini ninapaswa kuzungumza kwao, ilinibidi nirejee uzoefu wa maisha yangu binafsi, kupitia simulizi za safari ya uongozi waliopitia viongozi mbalimbali waliofanya mambo makubwa duniani, kupitia vitabu mbalimbali vya Uongozi na hatimaye nikajikuta nimeandaa mada niliyoiita kwa jina la “Ladder of Leadership for the Next Generation Leaders” (Ngazi ya Uongozi kwa Kizazi cha Viongozi wa Kesho).

Katika Mada hii niliainisha mambo 10 ambayo kijana anapaswa kuyazingatia ili aweze kufikia kiwango cha mafanikio katika uongozi au katika nyanja ambayo yeye anataka kuifanyia kazi. Baadhi ya mambo hayo ni muhimu siyo tu kwa viongozi vijana wa kesho bali ni muhimu kwa kila kiongozi ambaye anahitaji kufikiwa kiwango cha juu cha mafanikio ya uongozi wake.

Aidha, nimekuwa nikikutana na maswali kutoka kwa vijana wenzangu kwamba wana ndoto za kuwa viongozi wazuri na kuleta impact kwa jamii lakini hawajui wanafikaje na wanaanzia wapi?

Maoni yangu kwao ni kwamba hakuna single approach ya kufikia malengo ya kuwa kiongozi mzuri katika jamii. Ukisikiliza na kufuatilia safari ya viongozi mbalimbali utabaini kwamba kila mmoja amefanikiwa kwa namna tofauti na mwingine. Aidha, waandishi na wataalamu mbalimbali kuhusu Uongozi nao wanatofautiana katika dhana hii. Hata hivyo, wote wanakubaliana katika baadhi ya mambo ambayo mtu yeyote lazima ayazingatie ili kufikia katika mafanikio yake ya uongozi.

Kutokana na mahitaji ya maarifa ya uongozi kwa vijana kuwa makubwa, nimeamua kuandika #KITABU kuhusu mada hii ambacho inshaallah natarajia kukamilisha mwaka 2020, lakini kwa sasa nitakuwa nakupa sammary ya hatua hizo kumi "Ladder of Leadership for the Next Generation Leaders: 10 Steps to enrich your Leadership Potential".

Fuatana nami kupitia mitandao ya kijamii (instogram @jabiri_makame au subscribe YouTube Chanel  @Jabiri Makame au Like Facebook Page: Jabiri Omari – Young Visionary Servant Politician) Blog: http://jmakameyouthhub.blogspot.com/

Jabiri O. Makame
Governance and Leadership Expert
Chairman and Founder of Global Leadership Foundation
Mobile: +255 753276347 (whatsup) +255687672312

Comments

Popular posts from this blog

ARCHBISHOP TUTU FELLOWSHIP PROGRAMME FOR AFRICAN YOUNG LEADERS 2019

The Yale Young African Scholars Program 2019 for Secondary School Students, is now open! Apply today!

GREAT TRIP TO SHANGHAI