UONGOZI NI MSINGI WA MAENDELEO..... #InsideStoryBook2020: LADDER OF LEADERSHIP FOR THE NEXT GENERATION LEADERS: 10 Steps to Enrich Your Leadership Potential

“Uongozi ni msingi au sharti kuu la maendeleo endelevu kwa nchi yeyote ile” Prof. Joseph Semboja

Wanazuoni wa Sayansi ya Siasa na Uchumi Prof. Daron A. na Prof. J. Robnson katika Kitabu chao Why Nations Fail: The Origin of Power, Poverty and Prosperity wamefanya uchambuzi linganifu wa maendeleo baina ya nchi mbalimbali duniani. Matokeo ya utafiti wao kuhusu utofauti wa kiwango cha maendeleo kati ya nchi hizo, yanaeleza chanzo cha umasikini na utofauti wa kiwango cha maendeleo ni kutokana na taasisi zilizopo katika nchi husika, kwa maana ya taasisi za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Nchi zenye taasisi imara (strong institutions) zina kiwango kikubwa cha maendeleo ukilinganisha na nchi zenye taasisi dhaifu (weak institutions). Taasisi imara ndiyo kichocheo cha maendeleo endelevu na taasisi dhaifu ni kikwazo cha maendeleo.

Taasisi hizi hazijitengenezi zenyewe bali zinajengwa na kuimarishwa na #VIONGOZI. Uongozi una determine aina ya taasisi za nchi husika. Mathalani nchi za Asia (Four Asian Tigers) Singapore, Hong Kong, Korea ya Kusini na Taiwan, miaka ya 1960s kiwango cha maendeleo  kilishabihiana na nchi nyingi za Afrika. Lakini katika kipindi cha miongo 4 zimepiga hatua kubwa ya maendeleo ukilinganisha na nchi nyingi duniani. Msingi wa maendeleo yao yalitokana na #UONGOZI #PoliticalLeadership

Uongozi ni muhimu siyo tu kwa Taifa bali hata katika taasisi zetu katika sekta ya umma na sekta binafsi ambazo huchochea maendeleo. Mafanikio ya Taasisi hizi hutegemea aina ya viongozi wanaoziongoza. Kampuni kubwa duniani kama vile Microsoft, Apple, Alibaba na zingine ambazo zinatoa mchango mkubwa katika uchumi wa duniani zimefikia hapo kwa sababu ya uongozi madhubuti. Unapozungumzia mafanikio ya Kampuni ya Metl Group, Kampuni za Bakhresa, Clouds Media, IPP media na zingine ni kwa sababu ya uongozi Madhubuti #BussinessLeadership

Hata hivyo, msingi wa uongozi bora wa kuongoza Taifa na kuongoza taasisi mbalimbali ndani ya sekta ya umma na sekta binafsi, pamoja na kupata watu wanaoweza kufanya mambo makubwa katika Taifa inategemea uwekezaji katika kuwaandaa viongozi.  Uongozi ni mchakato wa maandalizi

John Maxwell anaeleza kwamba "kiwango cha mafanikio yetu katika jambo lolote kunategemea kiwango cha uwezo wetu katika uongozi" Hivyo, hata kiwango cha mafanikio ya maendeleo yetu kama Taifa na jamii inatokana na kiwango cha uwekezaji wetu katika kuandaa watu wenye uwezo wa kufanya mageuzi katika jamii.

Hivyo, ni muhimu sana kujenga kizazi chenye #LeadershilMindset kinachoweza kufanya mambo makubwa kwa maisha yao, katika sekta binafsi, sekta ya umma na taifa kwa ujumla.

Kwa vijana wenzangu, mafanikio yetu yanatokana na kiwango cha uwezo wetu katika uongozi. Uongozi wa kuongoza maisha yetu ambao ndiyo msingi wa kuongoza jamii na kuongeza thamani yetu kwa maendeleo ya Taifa.

Katika mfululizo wa Makala hizi nitakuletea muhtasari wa #Kitabu: NGAZI YA UONGOZI KWA KIZAZI CHA VIONGOZI WA KESHO: Hatua 10 za Kukuza Uwezo Wako wa Uongozi.

Fuatana nami kupitia Histogram @jabiri_makame Facebook Page: jabiri Omari-Young Servant Politician Blog: http://jmakameyouthhub.blogspot.com/

Ulizaliwa Kuwa Kiongozi, iishi Ndoto Yako.
#YouWereBornToLead #CherishYourDream

Comments

Popular posts from this blog

ARCHBISHOP TUTU FELLOWSHIP PROGRAMME FOR AFRICAN YOUNG LEADERS 2019

The Yale Young African Scholars Program 2019 for Secondary School Students, is now open! Apply today!

GREAT TRIP TO SHANGHAI