Posts

Showing posts from December, 2019

UONGOZI NI MSINGI WA MAENDELEO..... #InsideStoryBook2020: LADDER OF LEADERSHIP FOR THE NEXT GENERATION LEADERS: 10 Steps to Enrich Your Leadership Potential

Image
“Uongozi ni msingi au sharti kuu la maendeleo endelevu kwa nchi yeyote ile” Prof. Joseph Semboja Wanazuoni wa Sayansi ya Siasa na Uchumi Prof. Daron A. na Prof. J. Robnson katika Kitabu chao Why Nations Fail: The Origin of Power, Poverty and Prosperity wamefanya uchambuzi linganifu wa maendeleo baina ya nchi mbalimbali duniani. Matokeo ya utafiti wao kuhusu utofauti wa kiwango cha maendeleo kati ya nchi hizo, yanaeleza chanzo cha umasikini na utofauti wa kiwango cha maendeleo ni kutokana na taasisi zilizopo katika nchi husika, kwa maana ya taasisi za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Nchi zenye taasisi imara (strong institutions) zina kiwango kikubwa cha maendeleo ukilinganisha na nchi zenye taasisi dhaifu (weak institutions). Taasisi imara ndiyo kichocheo cha maendeleo endelevu na taasisi dhaifu ni kikwazo cha maendeleo. Taasisi hizi hazijitengenezi zenyewe bali zinajengwa na kuimarishwa na #VIONGOZI. Uongozi una determine aina ya taasisi za nchi husika. Mathalani nchi za Asia (Four...

NGAZI YA UONGOZI KWA KIZAZI CHA VIONGOZI WA KESHO: Hatua 10 za Kukuza Uwezo Wako wa Uongozi (LADDER OF LEADERSHIP FOR THE NEXT GENERATION LEADERS: 10 Steps to enrich your leaderahip potential)

Image
Kwa miaka kadhaa sasa nimekuwa nikikutana na vijana wenzangu katika matukio mbalimbali kuzungumza kuhusu masuala ya Vijana na Uongozi. Mwaka 2018  nilialikwa na Taasisi ya AmaniFursa katika kongamano liitwalo “Career Building Festival” kwenda kuzungumza na vijana wa sekondari kuhusu “Vijana na Uongozi” Baada ya kutafakari kwa muda kuhusu nini ninapaswa kuzungumza kwao, ilinibidi nirejee uzoefu wa maisha yangu binafsi, kupitia simulizi za safari ya uongozi waliopitia viongozi mbalimbali waliofanya mambo makubwa duniani, kupitia vitabu mbalimbali vya Uongozi na hatimaye nikajikuta nimeandaa mada niliyoiita kwa jina la “Ladder of Leadership for the Next Generation Leaders” (Ngazi ya Uongozi kwa Kizazi cha Viongozi wa Kesho). Katika Mada hii niliainisha mambo 10 ambayo kijana anapaswa kuyazingatia ili aweze kufikia kiwango cha mafanikio katika uongozi au katika nyanja ambayo yeye anataka kuifanyia kazi. Baadhi ya mambo hayo ni muhimu siyo tu kwa viongozi vijana wa kesho bali ni mu...